Wednesday, May 6, 2015

Juventus yaichapa Real Madrid 2-1

tevez
Na. Richard Bakana-shaffihdauda.com
Klabu bingwa barani Ulaya usiku huu imeendele kwa mchezo mmoja kati ya Juventus kutoka Italia pamoja na Real Madrid ya Spain ambapo Muargentina ambaye aliachwa katika fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, Carlos Tevez akiihakikishia timu yake ushindi wa Bao 2-1.

Katika mchezo huo Juventus ndio walianza kupata bao katika dakika ya 8 kupitia kwa Morata bao ambalo halikudumu sana kwani kunako dakika ya 27 Mreno Cristiano Ronaldo akasawazisha bao akiunganisha krosi safi ya James Rodriguez nakufanya timu hizo zinaenda kupumzika zikiwa 1-1.(P.T)
cr7 2
Baada ya kipindi cha pili kuanza Tevez ambaye kwasasa anafanya vyema kwa kucheka na nyavu, katika dakika ya 57 akaiandikia Juventus bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United pamoja na Manchester City kufanyiwa madhambi na kuangushwa ndani ya 18 na beki wa Real Madrid Carvajal.
cr7
Vikosi vya timu zote mbili vilikuwa kama ifuatavyo.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Sturaro, Vidal, Tevez, Morata
Subs: Storari, Barzagli, Padoin, Pepe, Pereyra, Llorente, Matri.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo, Ramos, Kroos, Rodriguez, Isco, Bale, Ronaldo.
Subs: Keylor Navas, Coentrao, Hernandez, Lucas Silva, Arbeloa, Jese Rodriguez, Illarramendi.
juve

No comments:

Post a Comment