AMAZING! Hiyo
ndiyo kauli pekee unayoweza kuitamka kuakisi shoo baab’kubwa
aliyoifanya mkali wa wimbo wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
London, Uingereza, Risasi Mchanganyiko linakujuza zaidi.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipagawisha wakazi wa jiji la London.
Shoo hiyo
iliyoacha gumzo la aina yake nchini humo kutokana na kupata idadi kubwa
ya mashabiki, ilifanyika Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Royal
Regency, maeneo ya Manor Park.
Chanzo
chetu kilichoambatana na msafara wa Diamond kwenye shoo hiyo ijulikanayo
kama Diamond are Forever, kiliweka bayana kuwa shoo hiyo ilikuwa ya
kustaajabisha (amazing) kwani ilikadiriwa kuwa na watu zaidi ya 1500
ambao ni Wabongo waishio nchini humo waliochanganyika na wazungu.
Akitambulishwa mbele ya mashabiki.
“Jamaa
kapiga shoo ya nguvu, watu walijaa kweli, si Wabongo pekee bali Wazungu
nao walikuwepo. Si zile shoo za kupiga sebuleni ambazo wasanii wengi wa
Kibongo huwa wanafanya. Yani hadi leo (Jumatatu) kila mtu anaizungumzia.
Imeacha gumzo la aina yake.
“Ilikuwa
yenye hadhi maana kiingilio kilikuwa ni shilingi laki moja na ishirini
kwa V.I.P na elfu tisini viti vya kawaida, Wazungu walichanganyikiwa
hadi ikabidi waulize Who is Diamond? (Diamond ni nani?) wakaambiwa na
meneja wa msanii huyo, Babu Tale kuwa ni msanii anayeiwakilisha Tanzania
akitokea Tandale, Dar es Salaam,” kilimwaga data chanzo hicho.
Mbali na umati huo ‘kuinjoi’ nyimbo za Diamond kama Kamwambie, Mbagala, Kesho na Nasema Nao na nyingine kibao, shoo hiyo iliongeza msisimko kufuatia uwepo wa balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Peter Kalaghe ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza machache jukwaani, burudani ikaendelea
No comments:
Post a Comment