Raia wa kigeni ashambuliwa Afrika Kusini
Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Polisi
walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati
kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto.
Msemaji
wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni
walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda
baadaye.
Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa.
Rais
Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku
ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency
Shirika
la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera
kwa nchi wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa
Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa.
Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.
Mhe.
Mkuya alichangia mada mbalimbali zilizohusu kundi hilo akilenga zaidi
maendeleo na muelekeo mzuri wa mafanikio ya kifedha katika nchi ya
Tanzania.
Waziri
wa Fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni Gavana katika mkutano
huu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande
wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni
Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Katika
Mkutano huu Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya juu na nguvu kubwa ya
kuweza kuyashawishi mashirika ya kifedha kuhusu nini kifanyike.
Mkutano huu uliofanyika leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa
na Shirika la Fedha la kimataifa katika kuimarisha taasisi za kifedha
katika nchi wanachama Afrika.
Katika
mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika
kundi hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia.
Wakijadiliana katika mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha
la kimataifa pamoja na taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza
masharti ya mikopo ili nchi wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya
kifedha kwa urahisi.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akishiriki katika mkutano huu wa kundi la Afrika. (African Group one Constituency)
Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia kwa karibu mkutano huu. (African Group one Constituency)
Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi la Afrika unavyoendelea. (African Group one Constituency)
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akifuatilia kwa karibu majadiliano ya
mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akichangia Mada katika mkutano huu wa kundi laAfrika. (African Group one Constituency).
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
15/04/2015.
MAFUNZO YA MAFUTA NA GESI ASILIA CHINA-SMZ
Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Mhandisi Mwalim Ali Mwalim na aliyevaa tai ni Mhandisi wa Idara ya Nishati, Omar Saleh Mohamed na wengine mwenye traksuti ni Afisa Mdhamini WQizara ya Ardhi, Makaazi Maji na Nishati Pemba, Mhandisi wa Miamba, Hemed Salim.
Maafisa
Waandamizi wa SMZ wakiwa viwanja vya Tiananmen Square wa mbele kabisa ni
Mkurugenzi wa Usalama kazini, Mhandisi Suleiman Khamis kushoto ni
Mwandishi wa habari Juma Mohammed na kulia ni Mhandisi wa Idara ya
Nishati, Omar Saleh Mohamed.
Maafisa Waandamizi wa SMZ wakiwa katika viwanja vya Tiananmen Square Jijini Beijing China. Maafisa hao wanahudhuria mafunzo ya muda mfupi ya mafuta na gesi asilia
Waziri Membe ziarani nchini Kuweit
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwasili
hotelini nchini Kuwait kwa ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo
atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait na
Mkurugenzi Mkuu wa Kuwait Fund.Anayeongozana na Waziri Membe (mwenye
kanzu nyeupe) ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Nassem Ibrahim Al
Najib ambaye alimpokea uwanja wa ndege.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao
kwenye nchi ya Kuwait na Tanzania. (Wa kwanza kushoto) ni Mhe. Prof.
Abdillah Omari, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait mwenye makazi yake
Saudi Arabia na (kulia) ni Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, Balozi wa
Kuwait nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ujumbe wake wakimsikiliza Mhe. Najib na kuangalia picha za viongozi mbalimbali wa Kuwait
No comments:
Post a Comment