Wachimbaji
wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na
kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka
kwa mashimo hayo katika kijiji cha Karore,Kata ya Runguya,tarafa ya
Msalala Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyang a.
Kamanda wa polisi mkoani humo,JUSTUS
KAMUGISHA a mesema kwa siku za karibuni wachimbaji hao wali acha
kuchimba kutokana na machimbo yalikuwa hayaonekani,lakini juzi kuna
mchimbaji mmoja aliona kuna dalili za kuonekana kwa machimbo hayo na
ndipo akawapigia wenz ake simu kwa ajili ya kwenda kuanza shughuli za
uchimbaji lakini ilivyofika jana shughuli hizo zilisitishwa.
Kwamujibu wa Kamanda KAMUGISHA,usiku
wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo
yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya
uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua
iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na
kusababisha vifo vyao.
Amesema miili tayari imeshat olewa
kutoka kwenye mashimo hayo,lakini bado wanaendelea na juhudi za
kuangalia kama kuna miili mingine imebakia
No comments:
Post a Comment