Mwanajeshi
akipita katikati ya waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya vijana
na askari polisi, Bujumbura Aprili 27 mwaka 2015. Jeshi linabaini kwamba
" linalindia usalama raia".
Na RFI
Viongozi
nchini Burundi wamechukua uamzi wa kufunga kituo cha redio RPA, moja ya
redio za kibinafsi inayosikika na watu wengi nchini humo, na katika
baadhi ya maeneo ya nchi jirani.
Redio RPA
kama redio za kibinafsi nchini Burundi zimekua zikitangaza moja kwamoja
kuhusu hali inayojiri wakati huu mjini Bujumbura, hususan maandamano
yanayoendelea. Serikali ya Burundi inaituhumu redio RPA kuendesha
propaganda kwa waandamanaji. Wakati huohuo mwanaharakati wa haki za
binadamu, Pierre-Claver Mbonimpa amekamatwa na polisi, na kwa sasa
haijulikani alipo. Hata hivyo hati za kuwakamata viongozi wa mashirika
ya kiraia zimetolewa
No comments:
Post a Comment