In Summary
Chelsea haina haraka ya kumrudisha uwanjani Costa
kwa hofu kuwa anaweza apate maumivu zaidi, lakini mwenyewe anataka
kucheza mchezo huo dhidi ya Arsenal. Fowadi huyo hakumaliza mechi na
Stoke City baada ya kuumia
HUU sasa unoko. Straika, Diego Costa amesema atajikaza na kuweka
kando maumivu yake ya misuli ili kuhakikisha anacheza dhidi ya Arsenal
katika mchezo ambao Chelsea inaamini ndiyo utakuwa mwisho wa mbio za
ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Chelsea haina haraka ya kumrudisha uwanjani Costa
kwa hofu kuwa anaweza apate maumivu zaidi, lakini mwenyewe anataka
kucheza mchezo huo dhidi ya Arsenal. Fowadi huyo hakumaliza mechi na
Stoke City baada ya kuumia.
Kocha Jose Mourinho alimfuta fowadi huyo kwenye
kikosi chake kwa wiki mbili kwa maana kwamba atakosa mechi dhidi ya
Queens Park Rangers na Manchester United huku kocha huyo Mreno akiwaza
pia uwezo wa kikosi chake kwenye safu ya ushambuliaji kucheza bila ya
staa huyo licha ya sasa kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba.
Arsenal kama itateleza kwenye mechi ya wikiendi
hii dhidi ya Burnley itaipa nafasi Chelsea kimahesabu kujisogeza kwenye
ubingwa kabla ya kwenda kumenyana nao Aprili 26, lakini kama tu watakuwa
wamezishinda QPR na Man United.
Hata hivyo, hata kama Arsenal wataichapa Burnley
kuna imani kubwa Stamford Bridge kwamba ushindi watakaopata Emirates
utawasogeza kwa asilimia kubwa kwenye ubingwa kitu ambacho Costa anataka
kuwamo kwenye mchezo huo.
No comments:
Post a Comment