Staa kutoka nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’,
Khadija Maige ‘Kadja Nito’, hatimaye ameamua kufunguka na kusema kuwa,
kwa maisha yake ya sasa ya kimuziki haoni kama kuna umuhimu wa kufikiria
masuala ya kuolewa.
Akizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Kadja
alisema kuwa, muziki sasa ndiyo kila kitu kwake hivyo hawezi kumpa
nafasi mwanaume au kuzungumzia suala la ndoa hivi sasa.
“Naweza kuishi maisha yangu bila mwanaume, napata mshiko, nawasaidia
ndugu zangu na mimi najimudu, mume wa nini maisha haya? Sasa ni muziki
na mimi, mimi na muziki, mapenzi yasubiri,” alisema Kadja.
No comments:
Post a Comment