Tuesday, April 14, 2015
wapendao blog
Mama mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini
Mwanza (jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume
na kisha kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni
jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa
viongozi wa serikali aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:
“Mimi ni mfanya usafi hapa Mkuyuni, wakati ninaenda kumwaga uchafu
pale dampo nikakuta kitoto kichanga kimetupwa maeneo hayo ndipo
nilipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Sokoni ili
wafanye utaratibu wa kukitoa hapo:”
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mkuyuni, Godwin Peter Kyangara, amesema:
“Mimi nimeletewa hizi taarifa za mtoto huyu aliyetupwa maeneo haya mida
ya saa 2:30 asubuhi, baada ya kupokea taarifa hizo ikabidi nikatoe
taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo walipokuja kuuchukua mwili wa mtoto
huyo.”
Inasemekana kwamba mtoto huyo alikuwa tayari ana umri wa miezi tisa
hivyo mzazi wake alikuwa tayari amejifungua ndipo alipoamua kumtelekeza
kwenye shimo hilo la kutupa takataka.
Kwa upande wake, diwani wa kata ya Mkuyuni, Charles Fashion, ameeleza
kuwa ameshangazwa na kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mtoto na
kumtupa jalalani ambapo alisema inabidi atafutwe na apewe adhabu iwe
fundisho kwa akina mama wengine wenye tabia kama hizo katika jamii.
Aidha, Jeshi la Polisi jijini Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa bado juhudi za kumtafuta mwanamke huyo aliyetenda
unyama huo zinaendelea ili afikishwe mahakamani kujibu mashtaka
yanayomkabili.
Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
No comments:
Post a Comment