Mbunge
wa Jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo akimtambulisha Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary kuwa mrithi wake wa kiti cha ubunge
katika jimbo hili wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba.
Ndesamburo akizungumza na wananchi wa Moshi mara baada ya kumtangaza mrithi wake katika jimbo la Moshi mjini.
.jpg)
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
akibadilishana mawazo na Bw. B. Lynn Pascoe ambaye ni kati ya wajumbe 14
wa Tume Huru iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya
tathmini kuhusu hali ya sasa ya Operesheni za Ulinzi wa Amani pamoja na
Misheni Maalum za Kisiasa. Tume hiyo huru iliyoteuliwa mwishoni mwa
mwaka jana imekwisha anza kazi.
Jana (
Jumatano ) Baadhi ya wajumbe wa Tume hiyo akiwamo Bw. Pascoe walikutana
katika majadiliano yasiyorasmi na Wawakilishi wa Kamati Maalum ya Nne ya
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kubadilishana mawazo kuhusu masuala
ya jumla yahusuyo Misheni Maalum za Kisiasa. Mkutano huo uliandaliwa na
Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa.
Akichangia
majadiliano hayo, Balozi Manongi, amesema kwamba Misheni Maalum za
Kisiasa, pamoja na umuhimu wake na mchango wake katika mustakabali wa
amani na usalama, lakini ni misheni ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na
nchi wanachama, hasa kutokana na ukweli kwamba uundwaji wake hauko wazi,
si shirikishi wala jumuishi.
Kutokana
na mazingira hayo, Balozi Manongi ameishuri Tume hiyo Huru kuliangalia
kwa mapana suala la Misheni Maalum za Kisiasa ikiwa ni pamoja na muundo
wa uundwaji wake na pia kuboresha uwazi, uwajibikaji na uwakilishi
utakaozingatia uwakilishi jumuishi wa kila kanda.
No comments:
Post a Comment