Tuesday, April 28, 2015
WAMILIKI wa Mabasi yaendayo mikoani wameitunishia misuli Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA )na kusema kuwa hawatashusha nauli kutokana na bei ya mafuta kupanda.
Wamesema kama SUMATRA hawatatoa majibu mapema kuanzia Aprili 29 mwaka huu hawatokata tiketi kwa wasafiri na badala yake wataendelea na mgomo huo kwa siku saba.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam jana katika kikao cha dharura cha wamiliki wa
mabasi yaendayo mikoani , Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema
SUMATRA ilikurupuka kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuda.
Wamiliki
hao waliafikiana kuwa yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara
kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za
kisheria.
TABOA
wameitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani
kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita
kwasababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha
bei ya mafuta kushuka
No comments:
Post a Comment