“Tofauti na jinsi nilivyo, mimi siko hivyo kabisa katika mambo ya mapenzi mambo ya ubabe hayana nafasi kabisa kwangu,” alisema Darleen
WIVU WA MAPENZI
WASABABISHA MAUAJI YA KUTISHA DAR, MFANYABIASHARA WA MWANZA AUA DADA WA
MPENZI WAKE, AJERUHI WENGINE NA KUJIPIGA RISASI NA KUFA PAPO HAPO
Majeruhi wa tukio la mauaji ya wivu wa mapenzi, Francis Shumila, akiwa
chumba cha dharura Taasisi ya Mifupa (MOI), Dar es Salaam leo asubuhi,
muda mfupi baada ya kufikishwa toka eneo la tukio Klabu ya Wazee Amana
Ilala,alikoshambuliwa na mfanyabiashara wa jiji la Mwanza, Gabriel Munis
aliyetaka kumuua anayedaiwa kuwa mpenzi wake Christina Alfred,lakini
akamuua dada ya mpenzi wake huyo, kujeruhi watu watatu na kisha kujiua
kwa kujipiga risasi.
Gari namba T 537 CJY aliyokuwa amepanda mpenzi
wake huyo pamoja na jamaa zake inavyoonekana
baada ya kushambuliwa na risasi.
Kumradhi kwa picha hii. Huyu ndiye bwana Gabriel Munis
baada ya kujiua.(Imeandaliwa na www.mwaibale.blogspot.com)
Na Dotto Mwaibale
SAKATA la mauaji yanayotokana na wivu wa mapenzi limeendelea kulisakama
Jiji la Dar es Salaam ambapo sasa mfanyabiashara Gabriel Munis (30-35)
amemwua kwa risasi mdogo wa mpenzi wake, kisha kujimaliza mwenyewe.
Mfanyabiashara huyo wa mkoani Mwanza, alifikia hatua ya kujiua kwa kile
kinachodaiwa kuwa alikuwa akidhani watu aliowamiminia risasi wote
walikuwa wamefariki dunia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Marietha
Minangi akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo mchana, alisema
tukio hilo lilitokea jana saa 1:00 asubuhi eneo la Klabu ya Wazee Amana
karibu na Hospitali ya Amana.
Kamanda Minangi alifafanua kuwa jana asubuhi Chritina ambaye ndiye
alikuwa mpenzi wa Gabriel alikuwa ndani ya gari pamoja na mama yake
mzazi Helena Eliezer, mdogo wake Alfa (34) (ambaye ni marehemu sasa) na
dereva Francis walikuwa wanatoka ndani ya geti la nyumba waliyokuwa
wakiishi.
Alibainisha kuwa baada ya kutokeza nje ya geti hilo ndipo walimkuta
marehemu ambaye ghafla alianza kuwamiminia risasi iliyompata Francis
begani na kichwani huku Christina ikimpata mguuni sanjari na mama yake
huku na kumpiga mdogo wake ambaye alifariki dunia papo hapo.
Kamanda Minangi alisema baadaye marehemu alijipiga risasi na kufariki
papo hapo.
Alisema miili ya Alfa na Gabriel imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana
ambapo majeruhi hao hao wawili walikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH).
Alisema Christina alitibiwa katiak Hospitali ya Amana na kuruhusiwa huku
mama yake na dereva walikimbizwa katika Hospitali Muhimbili huku
Francis hali yake ikidaiwa kuwa mbaya.
Mmoja wa ofisa wa jeshi la polisi ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa
kuwa si msemaji alisema Munis alikutwa na magazini mbili na
aliwafyatulia lisasi 14 na kuwa inaonesha kabla ya tukio hilo huenda
kulikuwa na mtu aliyekuwa akiwasiliana naye.
Alisema walioshambuliwa katika tukio hilo ni familia moja inayodaiwa
ilikuwa ikimsindikiza Christina aliyekuwa akienda nchini Cyprus.
"Habari ambazo hatuna uhakika nazo zinadai kuwa Christina alikuwa
akienda uwanja wa ndege kwa safari ya kwenda katika nchi hiyo" alisema
ofisa huyo.
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tukio jingine kama
hilo kutokea eneo la Kibamba Dar es Salaam mwezi uliopita.
Katika tukio hilo Anthery Mushi alimpiga risasi mama mazazi wa mpenzi
wake Ufoo Saro Mtangazaji wa Kituo cha televisheni cha ITV kisha
kumjeruhi Ufoo na kujiua mwenyewe akidhani alikuwa ameshawaua wote.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
No comments:
Post a Comment