Watu
watatu wameuawa na wengine kumi na sita ikiwa ni pamoja na wanajeshi
tisa wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga
dhidi ya kambi moja ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa,
kaskazini mwa Mali.
Shambulio
hilo limetokea kwenye umbali wa kilomita 90 kusini mashariki mwa mji wa
Gao. Wakati huohuo, katika mji mkuu wa Algeria, Algiers wawakilishi wa
makundi ya waasi wamekua wakijaribu kuzungumza na wasuluhishi wa
kimataifa na kueleza kwanini wameendelea kutupilia mkataba wa amani
uliyopendekezwa na timu ya usuluhishi.
Shambulio
limetokea kwenye saa tano na nusu mchana Jumatano wiki hii, wakati gari
moja lilikua likiendeshwa kwa kasi likielekea kwenye kambi ya wanajeshi
wa kikosi cha Umoja wa Mataifa ya Ansongo, katika jimbo la Gao,
kaskazini mwa Mali.
Wanajeshi
wa kikosi cha Umoja wa mataifa walilifyatulia risasi gari hilo
wakijaribu kulizuia lisiingie katika kambi yao. Wakati huo mtu aliyekua
katika gari hilo alijilipua, na kusababisha vifo vya watu watatu na
kuwajeruhi watu wengine saba. Wanajeshi tisa wa kikosi cha Umoja wa
Mataifa wamejeruhiwa vikali, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wawili ambao
wako katika hali ya maututi. Majeruhi wamesafirishwa hadi hospitali ya
Sévaré.
Wakati
huohuo, mtu mwengine ameuawa katika mji wa Kidal, kaskazini mwa Mali.
Mfanyabiasha aliyekua akiendesha pikipiki alikanyaga bomu lililotegwa
ardhini. Ajali hiyo imetokea kwenye umbali wa kilomita 23 mashariki mwa
mji wa Aguelhoc, kwenye barabara ya Tigharghar.
Katika
mji wa Boni, katika jimbo la Mopti, wanajeshi watatu wa jeshi la Mali
wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye yuko katika hali ya
maututi, wakati gari waliokuwemo ilipokanyaga bomu lililotegwa ardhini.
No comments:
Post a Comment