Monday, April 27, 2015
Na Mwandishi wetu,Mpekuzi.
Baada ya Rais Kikwete kuingia alipokelewa na Mkuu ya Jeshi la Wananchi(JTWZ),Generali Davis Mwamunyange ambaye alimpeleka kukagua vikosi vya ulinzi na usalama.
Jeshi
hilo limeonekana kufanya maboresho katika gwaride la mwaka huu ambapo
waliandaa gadi 20 huku gadi 13 zikiwa nje ya uwanja na gadi 7 zikiwa
ndani.
Gadi
13 zilizokuwa nje ya uwanja zilivalia mavazi ya mazoezi (Combat)huku
wakiwa wamebeba vifaa vya kivita ambapo kati ya hizo,gadi 1 ilikuwa
kikosi maalum cha makomandoo na gadi iliyobaki ilikuwa kikosi maalum cha
wanamaji.
Gadi saba zilizobaki ndani kikiwamo na kikundi cha bendi walikuwa wamevaa mavazi rasmi ya gwaride.
Baada
ya rais Kikwete kuingia ndani alipokelewa na Mkuu wa Majeshi(CDF),
Davis Mwamunyange ambaye alimpeleka kukagua gadi saba zilizokuwa ndani
huku mizinga 21 ikilia.
Baada
ya kukagua, gadi hizo zilisogea mbele kwa hatua 15 kwa ajili ya kutoa
heshima zao kwa amiri jeshi mkuu na kuendelea kusimama ndani ya uwanja
huku wakisubili gadi zilizokuwa nje ziweze kupita mbele ya amiri jeshi.
Gadi 11 zilipita kwa mwendo wa pole huku gadi mbili moja ikiwa kikosi cha makomandoo na wanamaji zilipita kwa mwendo wa kasi.
Viongozi Wanena:
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwenye maadhimisho hayo, baadhi ya viongozi wakuu
wastaafu wa serikali walisema kuwa muungano huo unapaswa kuigwa na
mataifa mbalimbali.
Spika Mstaafu Pius Msekwa alisema vijana wana nafasi kubwa ya kuuenzi na kuendeleza muungano huo ili uweze kudumu miaka hamsini mingine.
“Sisi
tumestaafu, tunawaachia vijana ili waweze kuendeleza, hivyo basi
wanapaswa kuunga mkono na kuudumisha ili uweze kudumu miaka mia moja,”alisema Spika Mstaafu Pius Msekwa.
Alisema
licha ya muungano huo kupitia kwenye mawimbi yaliyoibua kero za
muungano, mpaka sasa wameweza kuyashughulikia na kubakisha mambo
machache ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi.
Akitolea
mfano wa baadhi ya nchi ikiwamo Gambia na Senegal ambazo zilishindwa
kudumisha muungano baada ya kujitokeza kwa migogoro ya hapa na pale.
Msekwa
alisema kuwa ili kuonyesha kuwa muungano ni jambo la muhimu, ametunga
kitabu maalum ambacho kimeelezea mambo mbalimbali yanayohusu muungano na
misingi imara ya kuuenzi.
Naye
Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema kuwa,
muungano huo umeweza kuleta mafaniko makubwa katika Nyanja mbalimbali
ikiwamo ya kiuchumi na kijamii.
Alisema hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuudumisha ili uweze kudumu miaka hamsini ijayo.
Alisema
katika kipindi hiki cha kuelekea kura ya maoni ya katiba
inayopendekezwa na uchaguzi mkuu, vijana wengi wanapaswa kujitokeza ili
waweze kujiandikisha na kupiga kura.
“Ushiriki
wa vijana kwenye kupiga kura kwa ajili ya katiba inayopendekezwa ni
muhimu, kwa sababu inaweza kusaidia katika uchaguzi mkuu,”alisema Butiku.
Mtu Mmoja Akamatwa
Mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikamatwa na wanajeshi kwa kujifanya ni afisa wa usalama wa taifa.
Kijana
huyo ambaye alionekana katika maeneo hayo akiwaongoza wananchi ili
waweze kuingia ndani ya uwanja alikamatwa baada ya kubainika kuwa ni
afisa feki wa usalama.
No comments:
Post a Comment