Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mhe. Haroun Ali
Suleiman amesema ipo haja kwa wasomi wa kiislamu kuchukua juhudi za
makusudi katika kuunga mkono harakati za uanzishwaji wa Mtaala wa
Epistemolojia ya Kiislamu kwani ndio mfumo pekee utakaowawezesha vijana
hao kwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea kutokea kila siku
Duniani.
Ameyasema
hayo wakati akifungua Warsha ya siku 3 ya kujadili utungaji wa Mtaala
wa Epistemolojia ya Kiislamu wa masomo ya Vyuo Vikuu uliofanyika katika
Chuo Kikuu cha Kumbumbu ya Abdurahman Al-Sumait kilichopo Chukwani,
Zanzibar.
Amesema
Dini ya Kiislamu ni neema kutoka Allah ambayo hutofautisha moja kwa moja
kati ya binadamu na viumbe vyengine, hivyo ni wajibu wa kila muislamu
kuthibitisha hilo kwa kuelewa Nyanja zote za uislamu zilizofungamana na
Quran na Sunna ambavyo ndio misingi mikuu ya Epistemolojia ya Kiislamu.
.jpg)
Mhe.
Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa
Tanzania akimkabidhi Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo
ya Nje wa Oman Ujumbe Maalum kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Sultani Qaboos bin
Said Al Said, Mtawala wa Oman.
.jpg)
Makabidhiano yakiendelea huku Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Ali Ahmed saleh akishuhudia.
.jpg)
Waziri Membe akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman.
Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amekabidhi ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Sultani Qaboos bin Said Al Said, Mtawala wa Oman.
Ujumbe huo maalum ulikabidhiwa kwa Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdulla, Waziri wa Mambo ya Nje na mwenyeji wa ziara ya Waziri Membe nchini Oman, kwenye ofisi za Wizara hiyo jijini Muscat, Oman Alhamisi Aprili 16, 2015.
Makabidhiano hayo ya kihistoria nchini hapa, yalishuhudiwa na Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Zanzibar , Mhe. Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania Oman, na viongozi wengine wa nchi zote mbili na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment