Ripoti
kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa
hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama Rais wa Burundi
Meja
Jenerali Godefroid Niyombareh(Pichani juu) amewaambia waandishi wa
habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi
itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpito.
Kulingana
na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza
imeon'golewa madarakani. Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua
hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya
tatu ya urais wa Nkurunziza.
Jenerali
huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza
alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Kwa
sasa rais Nkurunziza yuko nchini alipokuwa anatarajiwa kujumuika na
viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa
Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.
Rais Nkurunzinza alikuwa amepuuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.
Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya "Mapinduzi
No comments:
Post a Comment