Chelsea wakisherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa msimu wa 2014/15.
CHELSEA
wamekabidhiwa kombe lao baada ya mechi yao ya mwisho dhidi ya Sunderland
leo iliyomalizika kwa wababe hao kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho.(P.T)
Mabao hayo yamewekwa kimiani na Loic Remy aliyetupia mawili huku lingine likifungwa na Diego Costa kwa mkwaju wa penalti.
Drogba akishangilia ubingwa wa timu yake.
Kwa ushindi wa leo, Chelsea wamefikisha jumla ya pointi 87 mbali na kuwa tayari walikuwa mabingwa kabla ya ligi hiyo kumalizika.
Huku Chelsea wakitwaa ubingwa huo, timu za Hull City, Burnley na QPR zimeyaaga mashindano hayo kwa kushuka daraja
No comments:
Post a Comment