Tuesday, May 5, 2015
Mgomo Wa Madereva Umemalizika Mchana huu baada ya majadiliano ya muda mrefu na mkuu wa wilaya ya Kinondoni.
Akisoma makubaliano hayo mbele ya wenzake, kiongozi wa madereva
amesema kuwa madai yao yatatatuliwa ndani ya siku 7 kupitia
timu ya madereva iliyoundwa kushughulikia madai hayo.
Mabasi ya mikoani kutoka Ubungo sasa yameanza safari baada ya mgomo wa takriban siku 2.
Makubaliano yaliyofikiwa ni kuundwa kwa kamati ya madereva zaidi ya 8
watakaokutana na mkuu wa wilaya kuanzia kesho.
Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai yao kwa muda usiozidi siku 7 kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya Paul Makonda
Kamati iliyoundwa inatakiwa kujadili madai yao kwa muda usiozidi siku 7 kwa usimamizi wa mkuu wa wilaya Paul Makonda
No comments:
Post a Comment