Mwigulu Nchemba.
ALIYEKUWA
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba
amejiuzulu nafasi hiyo ili awanie nafasi ya kugombea urais na nafasi
yake imechukuliwa na Rajab Luhavi aliyekuwa mshauri wa rais katika
siasa.
Mwigulu
amabye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo
jana jioni katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani
Dodoma.
Akithibitisha
taarifa hiyo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema
kuwa Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na nia yake ya
kutaka kuomba kuwania urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
"Mwigulu
alikuwa ameshamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete,
naye akamkubalia, sasa jana katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na
mwenyekiti amemkubalia mbele ya wajumbe wa NEC" Alisema Nape.
Nape
amesema kufuatia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete amemteua
msaidizi wake katika masuala ya siasa, Ndugu Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe
wa NEC, na wakati huohuo kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM kushika
nafasi iliyoachwa na Mwigulu.
No comments:
Post a Comment