Monday, May 11, 2015

Pinda afungua maonyesho ya elimu Dodoma



PG4A2164
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Sista  Flosy Sequeire, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Saint Francis ya Mbeya tuzo maalum ya kutambua  ufalu mzuri wa wanafunzi wa shule  hiyo  wakati alipofungua  maadhimisho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Wemgne kutoka kushoto ni  Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A2337
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wiki ya elimu wenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15, 2015.  Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.
PG4A2343
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 1015. Kulia ni Bibi Agnes Israel.

No comments:

Post a Comment