Wednesday, May 20, 2015
Rais wa Msumbiji Fellipe Jacinto Nyusi jana amelihutubia bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema ziara yake imelenga kuja
kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili tangu enzi za
harakati za ukombozi.
Rais
Nyusi alisema hayo jana wakati alikilihutubia bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu
nchini ambapo alisema siku zote maendeleo ya nchi yanatokana na uhusiano
mzuri baina ya nchi na nchi.
Bw. Nyusi ambaye anakuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji kuhutubia bunge la Tanzania, alisema kuwa mbali na ushirikiano mzuri wa kisiasa angependa kuendeleza ushirikiano wa kibiashara, elimu na katika nyanja nyingine mbalimbali.
Rais Nyusi ambaye aliingia nchini Juzi ameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kisha akaelekea visiwani Zanzibar ambapo alikutana na Rais wa visiwa hivyo Dkt, Ali Mohammed Shein na jana alimalizia ziara yake Bungeni mjini Dodoma.
Katika hotuba, Rais Nyusi pia aliahidi kushirikiana na Tanzania katika ulinzi wa amani pamoja na vita dhidi ya ugaidi katika mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake spika wa bunge la Muungano Mh. Anne Makinda alisema kuwa ni heshima kubwa kwa Rais huyo wa kwanza wa msumbiji kuhutubia bunge na kuongeza wataendelea kukuza uhusiano baina ya nchi hizo ili kuleta maendeleo ya nchi hizo.
Makinda alisema kumekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa ambao kwa sasa wataendeleza mshikamano kati ya wabunge wa Tanzania na Msumbuji ili kuboresha maisha ya wananchi wa nchiu zote mbili.

No comments:
Post a Comment