Friday, May 15, 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM


Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.
Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment