Wagombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza
Viongozi
wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga
kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.
Waziri
Mkuu David Cameron ataahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya
mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband
ataahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi".
Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.
Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.
Naibu
mhariri wa BBC James Landale amesema wanasiasa, wapiga kura na vyombo
vya habari wanajaribu kufuatilia kwa kina uchaguzi huo, na kuwafanya
wengi kufuatilia kile kitakachotokea iwapo matokeo yatakuwa kinyume na
matarajio yao.
"Alhamisi, huenda isiwe mwisho wa mchakato huo wa uchaguzi," amesema.
"Huenda uchaguzi huo ukaenda katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja."
Katika habari nyingine za uchaguzi mkuu:
Mgombea
wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika
kinyang'anyiro cha uchaguzi huo baada ya kupigwa picha akimtishia
kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.
Kiongozi
wa Labour Ed Miliband amesema haamini kama chama chake kitakopa zaidi ya
ilivyokuwa mipango ya chama cha Conservative iwapo kitashinda
uchaguzi.CHANZO
No comments:
Post a Comment