West Brom
imewachabanga mabingwa ligi kuu ya England Chelsea jumla ya mabao 3-0
hali ambayo kwa sasa inaifanya klabu hiyo kukaa eneo salama zaidi dhidi
ya kushuka daraja.
Katika
mechi hiyo iliyochezwa, dimba la The Hawthons, Saido Berahino alikata
utepe wa magoli kwa kufunga goli la kwanza mnamo dakika ya 9,na pia
dakika ya 47 Berahino tena akaweka kimiani goli la pili kwa njia ya
penati ,baada ya kuangushwa na John Terry eneo la adhabu na hivyo hadi
mwisho wa mchezo West Brom 3 Chelsea mabingwa nunge. Kwa matokeo hayo
West Brom sasa wamefanikiwa kukaa eneo salama kuepuka kushuka
daraja,huku Chelsea wakiwa bado mabingwa. Kesho Arsenal watakwaana na
Sunderland.
No comments:
Post a Comment