Makadam na Prasad wakiwajibika
Wapenzi wakipigishwa mpumwende.
Baada ya
ziara ya mafanikio ya mwezi mmoja mjini Addis Ababa, bendi ya Swahili
Blues chini ya uongozi wa Leo Mkanyia imefanya ziara nyingine mjini
Nairobi.
Bendi
hiyo yenye maskani yake katika hoteli ya nyota tano ya Serena iliyo
katikati ya mji wa Dar es Salaam ilianza ziara yake katika klabu maarufu
inayojulikana kama Choices iliyopo katika barabara ya Baricho kwenye
kitongoji cha Industrial Area. Shoo hiyo kabambe ilifanyika siku ya
tarehe 23 April 2015 chini ya usimamizi wa kampuni maarufu ya Roots
International katika mradi maalumu uliojulikana kama Thursday Nite Live
@Choices kwa udhamini wa Tusker Malt Lager.
Shoo hii
ilifana vilivyo na wapenzi lukuki waliohudhuria walikunwa kisawasawa na
mirindimo kabambe toka kwa Swahili Blues Band. Wapenzi hao pamoja na
kukunwa ipasavyo na umahiri wa Leo vilevile walifurahishwa sana na
mwimbaji pamoja na mpiga ngoma Juma Setumbi. Kwa habari zaidi juu ya
shoo hii tafadhali tembelea tovauti hiiwww.facebook.com/thursdaynitelive
No comments:
Post a Comment