Thursday, June 4, 2015

HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR KUTOA HUDUMA SAA 24

Na Rahma Khamis /Takdiri Ali- Maelezo Zanzibar
Wizara ya Afya Zanzibar imesema Kitengo cha Mifupa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kinaendelea kufanya kazi zake za kutoa Matibabu Masaa 24 kama kawaida kwa kufuata utaratibu maalum uliowekwa Hospitalini hapo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua lini Serikali itaweka daktari katika Hospitali hiyo kwa Masaa 24.
Amesema Hospitali ya Mnazi Mmoja ni Hospitali Pekee ya Rufaa kwa Zanzibar ambayo inafanya kazi ya kutoa huduma bora za afya na kwamba kwa sasa ina Madaktari bingwa wa Mifupa Wawili wanaopatikana kwa muda wa Masaa 24

No comments:

Post a Comment