Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!
Wiki iliyopita zilisambaa picha mtandaoni zikimuonyesha Wema Sepetu akiwa amepozi
kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya
eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka
2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia
kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
Katika
maelezo yake kuhusiana na kusambaa kwa picha hizo, Wema amesema
kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani
yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu,
hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.
“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina
Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi,
naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua
maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na
mpenzi wa mtu!
No comments:
Post a Comment