Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi Irina Bokova.
DUNIA endelevu haiwezi kuwapo kama hakutakuwepo na bahari yenye kuendeleza uhai.
Miezi
michache kabla ya kufanyika kwa kongamano la kihistoria la COP21 (21st
Conference of the Parties to the United Nations Framework Convention on
Climate Change) la kutengeneza ajenda mpya ya maendeleo endelevu, ujumbe
huu ulikuwa hauna tija.
Lakini sasa ujumbe huu una tija sana na muhimu sana.
Iwe nchi
iko mbali na bahari au karibu, kila nchi na kila aina ya uhai hutegemea
zaidi namna bahari inavyokuwa salama na yenye kutekeleza wajibu wake wa
kulea uhai.
Kiukweli
bahari ni kitu muhimu katika mfumo wa hali ya hewa duniani, ikiratibu
kwa namna ya kipekee mabadiliko ya muda mrefu ya hali ya hewa na mfupi
na pia uwepo wa hewa mbalimbali katika anga ikiwemo oksijeni tunayovuta.
Aidha inawezesha kuwapo kwa lishe na kuwa chanzo cha chakula.
No comments:
Post a Comment