MTU kwao!
Licha ya kuwa staa wa muvi za Bongo, mwigizaji kiwango, Jacqueline
Wolper Massawe anadaiwa kuitwa na wazazi wake kwenda kuishi nyumbani
kwao, Kibaha mkoani Pwani ili kuepukana na skendo za kila mara za mjini.
Staa wa muvi za Bongo, mwigizaji kiwango, Jacqueline Wolper Massawe.
Kwa
mujibu wa chanzo, Wolper amewekewa msimamo huo na wazazi wake, hususan
mama yake mzazi aliyemwambia kwa kuwa ana usafiri anaweza kuishi huko na
kufika jijini Dar kwa kazi za mchana kutwa kisha kurudi Kihaba kwa
malazi na makazi.
Wolper
alipotafutwa kuulizwa kuhusu hilo, alijibu: “Kweli wazazi wangu
wanapenda niwe nao karibu wakiamini nitaendelea kuwa mtoto mzuri bila
skendo, lakini inakuwa ngumu ndiyo maana utakuta mara nyingi niko kule
lakini kimakazi niko Dar, nitafikiria.
No comments:
Post a Comment