Kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe ambaye ametua Simba msimu huu akitokea klabu ya Vicem Hai Phong F.C ya Vietnam Justice Majabvi ambayo alikuwa amemaliza mkataba wake katika klabu hiyo. Bado anaendelea kukupa ile exclusive interview aliyofanya na millardayo.com.
Majabvi amesajiliwa na Simba kwa kiwango kizuri alichokionyesha baada ya kufanya majaribio na klabu hiyo ila swali lilikuwa hivi mbona Majabvi ana kiwango kizuri ila rekodi zinaonesha mara ya mwisho kucheza katika timu ya taifa ya Zimbabwe ni mwaka 2012, tatizo nini?
“Ndio
niliacha kuchezea timu ya taifa kwa sababu ya matatizo mengi katika timu
ya taifa, nimecheza timu ya taifa toka mwaka 2004 hadi 2012, kwa sababu
ya matatizo binafsi na shirikisho la soka la Zimbabwe, nilikuwa natumia
hela yangu kama nauli kuja kucheza timu ya taifa lakini sikuwa
nikirudishiwa” >>> Majabvi
No comments:
Post a Comment