Na Bakari Kimwanga, Mwanza
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja
ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance
(ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema
haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema 'ni adui kwao'.
"Mtume
Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na
sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono
Ukawa halafu mnawakaribisha?
"Nendeni
kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni
niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA
mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya
kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa," alisema
Mnyika.
Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao.
Zitto ajibu
Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto
alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia
siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa
za upinzani.
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.
"Mwanzo
walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika,
tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa
upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya
kuiondoa CCM...wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua
watu gani hawataki kuiondoa CCM," alisema Zitto.
Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
"Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi," alisema na kuongeza:
"Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana...mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
"Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi," alisema na kuongeza:
"Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana...mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
"Tunakuja
na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi,
kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na
kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia," alisema Zitto.
Alisema
tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za
watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote
za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi Zitto
ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira,
waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia
wilayani Misungwi.
Mapokezi
hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha
wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi alipoingia
kwenye uwanja wa Furahisha
No comments:
Post a Comment