Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka
2015 ambazo Kitaifa zinafanyika Mkoani Ruvuma.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Waizri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt
Fenella Mukangara wakati wa mazoezi ya ya mwisho yaliyofanyika katika
Uwanja wa mpira wa Majimaji mjini Songea.
Waziri
Fenella amesema kuwa maandalizi yameenda vizuri na kuwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi katika sherehe hizo za uzinduzi wa mbuio za Mwenge
na kutoa hamasa zaidi kwa Vijana wotye nchini kushuhudia uzinduzi huo
ata kwa vile utaonyeshwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa
(TBC).
"Nisema
tu kuwa maandalizi yamekwenda vizuri sana mmejionea vijana wa Halaiki
walivyo onyesha umahiri wao, niwatate tu wakazi wa mjini wa Songea
mjitokeze kwa wingi kuja kushuhudia sherehe hizi za uzinduzi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru lakini pia VIjana nchini kote shuhudieni tukio hili
muhumu kwa kuwa litaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa TBC"
Alisema Dkt.Fenella
Aidha
Waziri Fenella alitoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa
wingi katika zoezi a kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura na
baadaye watumie demokrasia kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu
No comments:
Post a Comment