Friday, April 17, 2015
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga hivi karibuni ametoa ushuhuda wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujisaidia kitandani mpaka alipofika kidato cha pili lakini alipona katika mazingira ya kushangaza.
Akizu-ngumza na mwandishi wetu Lungi alifunguka: “Nikiri tu kwamba nilikuwa
kikojozi mpaka nafikia form two, nilikuwa naona aibu sana lakini
aliyenisaida ni bibi mmoja ambaye aliniponya katika mazingira ya
kushangaza.
“Baada ya kumwambia tatizo langu, aliniambia nipande kwenye
mti wa muembe nikiwa na nguo zangu, nikiwa juu akaniambia nikojoe kisha
nishuke.
“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu
limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo
sikujisaidia tena kitandani.”
No comments:
Post a Comment