Friday, April 17, 2015
Kura ya maoni ifanyike baada ya uchaguzi
Wakazi wa wilaya ya Muheza wameishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuahirisha zoezi la kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa na badala yake isubiri hadi uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge ufanyike.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na kituo cha sheria
na haki za binadamu kwa kushirikiana na tume ya taifa ya uchaguzi wakazi
hao wamesema mapendekezo mengi waliyowasilisha katika rasimu ya kwanza
ya katiba kwa mwenyekiti wa tume hiyo jaji Joseph Sinde Warioba
yamepunguzwa hivyo ni lazima tume ijipange upya ili kuleta Demokrasia ya
kweli nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wazee wa wilaya ya Muheza akielezea
suala ya uhesabuji wa kura mara baada ya ya siku ya upigaji kura kufika,
ameiomba tume ya taifa kufanya mabadiliko kwa waratibu wa uchaguzi
ambao ni wakurugenzi wa halmashauri katika mchakato huo na badala yake
watafutwe watu wa makundi tofauti yenye heshma kwa sababu watakosa imani
ya kupata takwimu sahihi za waliopiga kura ya hapana na ndio.
Kufuatia hatua hiyo mratibu wa kampeni ya utoaji elimu kwa wananchi
kuhusu Katiba Pendekezwa wa kituo cha sheria na haki za binadamu mkoa wa
Tanga Bwana Stanley Gumbo amewataka wananchi kuzingatia elimu ya katiba
zoezi hilo la kitaifa lengo lake ni kutaka wananchi wakubali kwa ridhaa
yao ili kupata Katiba mpya
No comments:
Post a Comment