Mahakama Kuu ya kenya.
Katika
hatua ya kushitua, Mahakama Kuu nchini Kenya imesalimu amri mbele ya
mashinikizo ya watetezi wa vitendo vichafu vya ulawiti, usagaji, ushoga
na kusema kuwa sasa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uasherati
wanaweza kusajili mashirika ya kile kinachodaiwa ni kutetea haki zao za
kibinadamu.
Majaji
watatu wa mahakama hiyo wameiamuru Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo
ya Kiserikali (NGOs) kulitambua na kulisajili shirika moja ambalo awali
mahakama hiyo ilizuia lisajiliwe kwa sababu za kimaadili na kidini.
Jopo
hilo la majaji Isaac Lenaola, Mumbi Ngungi na George Odunga limedai
kuwa, katiba ndio marejeo ya kila kitu nchini Kenya na kwamba serikali
haitakiwi kuzingatia mafundisho ya kidini katika maamuzi yake ambayo kwa
mujibu wa majaji hao, maamuzi hayo yananyima kundi fulani la watu uhuru
wao.
Uamuzi
huo umechukuliwa huku mashinikizo ya nchi za Magharibi dhidi ya nchi za
Afrika ya kuzitaka zitambue rasmi vitendo hivyo vichafu yakizidi
kupamba moto.
Nchi za Magharibi yametishia kuzinyima misaada nchi za Afrika iwapo hazitatambua rasmi vitendo vya ulawiti na usagaji.
Hatua
ya Mahakama Kuu ya Kenya imechukuliwa pia katika wakati huu wa
kukaribia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini Kenya ambaye ni
mtetezi mkuu wa vitendo hivyo vichafu
No comments:
Post a Comment