Shirika
la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani
kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye
ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika
manispaa ya Shinyanga. Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona
mbali(Telescope Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand
Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome
Magnifier)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani ya
ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye msimamizi
mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija
katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali (katikati),wa kwanza
kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima
Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez
wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34 vilivyotolewa na Shirika
la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona mbali(Telescope
Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza
Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)
.
Meneja wa
Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange akimkabidhi
vifaa hivyo na kushikana mkono na msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija
Peter Ajali
No comments:
Post a Comment