Wednesday, April 29, 2015

KAJALA APEWA SIKU 5 ZA KUISHI


Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.

Kajala Masanja akiwa kwenye pozi.
WALIKUWA KWENYE TOYOTA RAV 4
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watu hao wapatao watatu walitinga nyumbani hapo usiku huo mnene huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Rav 4 milango mitano rangi ya bluu ya kuiva na kumkuta mlinzi getini ambaye yupo kwa ajili ya kulinda usalama wa msanii huyo mwenye maadui kila kukicha."Walikuwa watano, walikuwa kwenye Rav 4 milango mitano, rangi ya blue ya kuiva. Wakamkuta mlinzi, walimuuliza kama Kajala yupo, mlinzi aliwadanganya kwamba hayupo."
MLINZI ALIJUA NI BWANA WA KAJALA
"Lakini mlinzi alidanganya akijua mmoja wa watu hao pengine ni bwana wa Kajala kwa hiyo ili kuua soo akasema hayupo lakini ukweli Kajala alikuwepo ndani. Yeye aliwaambia Kajala alikwenda kumsalimia mama yake, hajarudi.
WAACHA UJUMBE MZITO
"Ndipo mmoja wao akamwambia mlinzi kwamba, wao walikuwa na shida na Kajala lakini kwa sababu hayupo, wanaacha ujumbe apewe haraka sana. "Walisema akirudi aambiwe kuna watu walifika, wamempa siku tano za kuishi na kwamba wao wametumwa na mtu wa karibu na Kajala, lakini hawakumtaja kwa jina.
"Yaani mlinzi alitumia akili sana na kuwaambia Kajala hakuwepo ndani, alikwenda nyumbani kwao, ndiyo ilikuwa salama yake," kilisema chanzo hicho.
AMANI LAMSAKA KAJALA
Baada ya kuinyaka nyeti hiyo, Amani lilimsaka staa huyo na kumuuliza kama kuna ukweli wa madai hayo.
Awali, Kajala aligoma katakata kukubali akisema hajui lolote lakini alipobanwa zaidi na kuambiwa mlinzi wake ndiye aliyenyetisha habari hiyo, alikiri.
MSIKIE MWENYEWE
"Any way, ni kweli ishu imetokea usiku, lakini siyo saa nane, ilikuwa kama saa sita hivi. Mimi nilikuwa nimelala, nikaona simu yangu ikiita. Nilipoangalia ni mlinzi, nikapokea. Akaniambia kuna watu wamekuja, wamemwambia wametumwa waniletee ujumbe kwamba nimepewa siku tano za kuishi na wametumwa na mtu wangu wa karibu.
"Mimi sikuogopa, nilitoka hadi kwa mlinzi, lakini nilikuta gari imeshaishia zake. Kifupi ni kwamba katika watu si waoga ni mimi, unajua kwa nini? Naishi kwa kumtegemea Mungu sana. "Kwa hiyo siogopi japokuwa habari hizo zimenichanganya kupita kiasi, najiuliza ni mtu wangu gani wa karibu. Basi si mtu wa karibu bali ni adui yangu. Hivi hapa najiandaa kwenda Kituo cha Polisi Kijitonyama (Dar) kutoa taarifa kwa ajili ya tahadhari," alisema Kajala.
Akaongeza: "Unajua wiki yote iliyopita nilikuwa kwenye harakati za kumalizia filamu yangu ya Pishu. Kwa hiyo hata usiku wa jana nilichelewa kurudi, ile naingia tu nadhani ndani ya nusu saa ndiyo watu hao walikuja, kama ningechelewa zaidi huenda ningekutana nao getini."
ANAMHISI NANI?
AMANI: "Kajala wewe unajijua, unadhani nani anaweza kukutumia ujumbe kama huu miongoni mwa watu wako wa karibu?"
KAJALA: "Mh! Siwezi kumtaja hata kama kichwani yupo au wapo! Nitabaki kuwa na hisia zangu tu kwa sababu sina ushahidi. Ila kama ningewaona kwa sura hao watu na kuwatambua huenda ningeunganisha." Amani: "Huna mtu ambaye hivi karibuni mmetupiana maneno mabaya kwenye simu au laivu?" Kajala: "Sina. Mimi nipo na watu wangu ni amani tu na ndiyo maana nachangayikiwa." Mpaka tunakwenda mitamboni, Kajala alisema ndiyo amewasili kwenye kituo hicho polisi akisubiri kusikilizwa

No comments:

Post a Comment