Viongozi wa Ukawa Tanzania
Katika
kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimegawana
maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano ya hadhara na mafunzo kwa
viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa ushindi.
Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.
Chadema
kilianza ziara zake mikoani wiki zilizopita baada ya kuzindua mkakati
wake uitwao 'Hakuna kulala, Hakuna kula, Mpaka Kieleweke' nchi nzima
wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka kambi mkoani Kigoma kwa kile
ilichokiita kuimarisha majimbo ya kimkakati.
Sanjari
na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia katika moja ya ngome zake,
mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya kiushindi, kinahamasisha
wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.(P.T)
Jitihada
za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa ni majuma kadhaa tangu Chama
cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana
kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya mwaka 2010.
Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.
ACT -
Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kilihitimisha ziara yake ya
kimkakati katika mikoa tisa inayoonekana kuwa ngome ya CCM, wiki
iliyopita wilayani Bariadi, Shinyanga na kuvuna wanachama zaidi 6,000
katika mikoa hiyo.
NCCR-Mageuzi ipo Kigoma
Katibu
Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema jana kuwa Ukawa ina
mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya kuhakikisha inajiimarisha
kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.
Alisema
siku 10 zilizopita, timu ya NCCR ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti -
Zanzibar, Haji Hamis Hamad ilianza ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya
mkoa huo yanaendelea kuwa ngome yake.
"Kigoma
nzima ina majimbo yetu ya kimkakati na Ukawa wameshatukabidhi sasa
kilichobaki ni kufanya 'political management' (usimamizi wa kisiasa)
katika kiwango kinachotakiwa.
"Katika
kikosi hicho, pia wamo Katibu Mwenezi, David Kafulila, Katibu Mkuu
Mstaafu, Samuel Ruhuza na Kamishna wa Kagera, Peterson Mshenyela na
wengineo," alisema Nyambabe
No comments:
Post a Comment