Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hosea
Wakati
viongozi wajuu wa CCM wakiendelea kulalamikia makada wanaowatuhumu
kutumia fedha kujifagilia njia ya urais, mkurugenzi wa Takukuru, Dk
Edward Hoseah amesema taasisi yake inakusanya taarifa zote za wanachama
wa chama hicho tawala wanaotuhumiwa kutumia mlungula.
Mara
kadhaa viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakiwaonya wanachama wao dhidi ya
makada wanaotumia fedha kujitengenezea mazingira mazuri ya kupitishwa
na chama hicho kugombea urais, lakini wameeleza kuwa hawawajibiki
kuwaripoti Takukuru kwa kuwa ni wajibu wa chombo hicho cha kuzuia na
kupambana na rushwa kufanyia kazi malalamiko hayo.(P.T)
Jumatano,
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye
alisema Takukuru hawahitaji kupata mwaliko wa CCM ili kufanya uchunguzi
wa kukamata wagombea wanaotumia rushwa ndani ya chama hicho kwani rushwa
inayoendelea kwa sasa iko wazi.
"Kazi ya
kuwafuatilia imeshaanza muda mrefu, tunazo taarifa zao za kutosha kwa
kila mwanasiasa anayelalamikiwa," alisema Dk Hoseah wakati alipoongea na
gazeti hili kuhusu sababu za taasisi yake kukaa kimya wakati ikielezwa
hadharani kuwa rushwa imezidi katika harakati za uchaguzi ndani ya CCM
Dk Hoseah
alisema kwa muda mrefu Takukuru imekuwa ikifuatilia mienendo ya
wanasiasa wanaotaka uongozi kupitia chama hicho na ambao wanatuhumiwa
kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Alisema
Takukuru kwa sasa inaendelea na kazi yake ya uchunguzi dhidi ya tuhuma
hizo huku ikikusanya taarifa za kila mwanasiasa anayeonekana kutuhumiwa
na vitendo vya rushwa.
"Siyo
kwamba Takukuru haijaona wala haisikii malalamiko ya viongozi CCM.
Tunajua wajibu wetu na kazi ya kuwafuatilia imeshaanza," alisema Dk
Hoseah.
"Sheria
ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 imekataza wazi kwamba, ni makosa
kutoa chochote kama zawadi kwa kundi la watu, vinginevyo ni kukiuka
sheria hiyo. Labda kama anaonekana kuwa na fedha nyingi basi ajenge hata
barabara kuliko kufanya hivyo."
Dk Hoseah
aliongeza kuwa sheria pia inazuia kuanza kampeni kabla ya muda kupangwa
rasmi na Tume ya Taifa (Nec), kwa hivyo muda wa kampeni utakapoanza,
itarahisisha kukusanya taarifa zake na kuchukua hatua kwa wanasiasa hao.
"Kwanza
ni kosa kufanya kampeni kabla ya muda, lakini pia ni kosa kutoa zawadi
kama maji ya kunywa kama unafahamu kuwa wewe ni mwanasiasa
utakayegombea. Sheria yetu ya Takukuru inaweka wazi pia kitendo hicho ni
kosa," alisema Dk Hoseah.
Mapema
wiki hii, akiwa kwenye vikao vya ndani na viongozi wa chama hicho wa Dar
es Salaam, makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangulla alisema fedha
zinazotumiwa na makada kununua wanachama "kama maandazi", zitakuwa
kitanzi chao kwenye uchaguzi mkuu, akisisitiza kuwa wanachama hao
watang'olewa.
Mbali na
Mangula, wengine waliowahi kulalamikia rushwa ndani ya chama hicho ni
mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete ambaye alitahadharisha kuwa jambo hilo
linaweza kukiuangusha chama
No comments:
Post a Comment