Thursday, May 7, 2015

Mastar’ wa Afrika wamuunga mkono Adebayor.

LONDON, ENGLAND - FEBRUARY 09:  Emmanuel Adebayor of Tottenham Hotspur reacts during the Barclays Premier League match between Tottenham Hotspur and Everton at White Hart Lane on February 9, 2014 in London, England.  (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)
LONDON, ENGLAND – FEBRUARY 09: Emmanuel Adebayor of Tottenham Hotspur reacts during the Barclays Premier League match between Tottenham Hotspur and Everton at White Hart Lane on February 9, 2014 in London, England. (Photo by Shaun Botterill/Getty Images)

Siku chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Togo na klabu ya Tottenham Hotspurs Emanuel Sheyii Adebayor kufichua siri kadhaa nzito za familia yake , watu kadhaa maarufu barani humu wamejitokeza na kumuunga mkono katika sakata lake na familia yake ambalo limekuwa likiendelea kwa muda mrefu .
Adebayor ambaye aliandika mambo mengi katika waraka mrefu uliochapishwa kupitia ukurasa wake binafsi kwenye mtandao wa Facebook amejikuta akiungwa mkono na watu mbalimbali ambao wameeleza kumuonea huruma kwa kile kinachoonekana kuwa mzigo mzito unaomuelema kiasi cha kumfanya ashindwe kuzingatia kazi yake ya msingi ambayo ni kucheza soka.
Moja kati ya mapacha wanaounda kundi maarufu la muziki toka Nigeria la P-Square Peter amemuunga mkono Adebayor ambapo amemsifu kwa ujasiri wake na jinsi alivyojitokeza kuwa muwazi na kutoa yanayomsibu maishani mwake .

Mwanamuziki Peter wa kundi la P-Square amemuunga mkono Adebayor kwa kitendo chake cha kufichua mgogoro ulioko kati yake na familia yake .
Mwanamuziki Peter wa kundi la P-Square amemuunga mkono Adebayor kwa kitendo chake cha kufichua mgogoro ulioko kati yake na familia yake .
Peter amemuandikia Adebayor na kumwambia kuwa ‘Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayekudai lolote , familia yako inapaswa kuona fahari kuwa na mtoto kama wewe na si kinyume chake ‘.
Nyota wa zamani wa Arsenal Emmanuel Frimpong kwa upande wale aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter ambapo amesema kuwa baada ya kusoma kilichomsibu Adebayor anashukuru Mungu kwani familia yake ni kila kitu kwake .
Nyota wa Chelsea na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba naye alionyesha kumuunga mkono Adebayor ambapo amemwambia kuwa kuzungumza naye kumfundisha mengi na amemuombea kwa Mungu na anajua ipo siku familia ya Adebayor itarudi katika msingi wa familia zote ambao ni Upendo .

Nyota wa Chelsea Didier Drogba naye amejitokeza kumpa 'Support' Adebayor katika mgogoro wake na familia yake.
Nyota wa Chelsea Didier Drogba naye amejitokeza kumpa ‘Support’ Adebayor katika mgogoro wake na familia yake.
Didier Drogba ni moja kati ya watu ambao wamekuwa karibu na Adebayor katika kipindi hiki kigumu na inasemekana kuwa alizungumza na Adebayor saa chache kabla ya kuandika waraka mrefu kwenye mtandao wa Facebook .
Adebayor amefichua mgogoro mkubwa ulioko baina yake na ndugu zake pamoja na mama yake mzazi ambapo amesema kuwa sababu kuu yay eye kufanya hivyo ni kutoa funisho na picha alisi ya jinsi ambavyo familia za Afrika zina shinikizo kwa vijana waliofanikiwa .
Dada wa Adebayor anayefahamika kwa jina la Lucia amejibu mapigo ya waraka ulioandikwa na nyota huyo ambapo amesema kuwa kila kilichoandikwa na Adebayor ni uongo na kwa sasa familia yake haimhitaji

No comments:

Post a Comment