Unaweza kumuagiza mtu awapigie simu ndugu zako awape taarifa kwamba umefariki??
Nimeipata hii kwenye Hekaheka ambayo
imetokea Mabibo Dar.. mwanamke mmoja kaongea na ndugu yake akamwambia
awapigie simu ndugu wa mume wake kwamba yeye amefariki, kisa cha kufanya
hivyo amesema eti alitaka kuona kama ndugu wa mume wake kama
wanampenda.
Ndugu wakapata taarifa wakaanza taratibu
za kukusanya michango ya msiba, pamoja na taratibu nyingine za kwenda
kwenye msiba, wakakutana na ndugu ambaye alitoa taarifa kwao kwamba kuna
msiba wa mwanamke huyo.
Wakamtafuta mume wa mwanamke huyo, baada
ya kumpata wakaendelea na taratibu za kwenda msibani, kitu cha ajabu
yake baadae wakamkuta mwanamke huyo yuko kwa dada yake, mzima wala
hajafariki.
Ndugu hao wa mume waliamua kwenda Polisi
kuripoti lakini wakaambiwa warudi nyumbani kuimaliza hii ishu
kifamilia, Hekaheka yote iko kwenye hii sauti hapa.. bonyeza play
usikilize yote mtu wangu
No comments:
Post a Comment