Friday, May 22, 2015

NANI KUJINYAKULIA TUZO ZA FILAMU 2015 KESHO JUMAMOSI!

...
Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(katikati) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao katika ofisi zake kuelezea siku ya tuzo za filamu zitakazofanyika jumamosi hii jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Bwana Ezekiel kutoka Push Mobile na kushoto kwake ni Meneja Masoko wa EATV na EAR Happy Shame.

Meneja Masoko kutoka EATV na EA Radio Happy Shame(kulia)akielezea jambo kwa Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba wakati wa mkutano na wana habari kuhusu Tuzo za Filamu Tanzania 2015 leo jijini Dar es Salaam ambapo EATV na EAR ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo.
Mei 23, hapatoshi Mwalimu Nyerere Internnational Conference Center;

Ni siku moja tu imebaki kufanyika kwa tuzo kubwa za filamu nchini 'Tanzania Film Awards' 2015(TAFA). Ni tuzo kubwa ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei 2015, Mwalimu Nyerere International Conference Center. Haya ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini na kila mmoja ana shauku ya kushuhudia tuzo hizo zitakazo wapa wasanii wetu amsha amsha ya mafanikio katika tasnia yao.
Akiongea na wana habari katika ofisi zake raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba alisema, "Maandalizi yote yapo tayari na tumejipanga kikamilifu kufanikisha tuzo hizi. Kutakuwa na burudani mbalimbali kusherehesha tuzo hizi zikiongozwa na mzee Kikii, Mwasiti na Barnaba, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wana tasnia ya filamu watakaowakilisha vizuri kabisa tasnia yao kwa kutufanya tucheke na tufurahi.

No comments:

Post a Comment