Thursday, May 7, 2015

SUNGUSUNGU WA MANISPAA YA SHINYANGA WAPEWA PIKIPIKI



Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga, James Deshi.Pichani katikati ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.

Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.Matiro alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki kwa jeshi la sungusungu katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na viongozi wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga.
Viongozi wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama Malunde-

No comments:

Post a Comment