Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania,Magembe Makoye akizungumza
na wandishi wa habari kushusiana na wafugaji kufanya shughuli zao
kwa kufuata sheria za nchi katika ukumbi wa Habari MAELEZO leo jijini
Dar es Salaam kulia ni Mkurugezi Msaidizi wa Idara ya HABARI MAELEZO
Tiganya Vincent .
Baadhi ya waandishi wa habari
Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
CHAMA cha
wafugaji Tanzania (CCWT),kimewataka wafugaji wote nchini kufanya
shughuli zao kwa kufuata sheria, pia hawataki kuona wafugaji wakifanya
uonevu wa aina yoyote kwa watu wengine.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT),Magembe
Makoye wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari
MAELEZO leo jijini Da es Salaam.
Makoye
Amesema kuwa wafugaji watambue kuwa kunakutegemeana na watu wengine
katika kuendesha shughuli zao bila kuathiri watu wengine katika jamii.
Pia
Makoye amesisitiza kuwa chama cha wafugaji Tanzania hakitavumilia kuona
wafugaji wanakuwa chanzo cha migogoro katika jamii,aidha chama hicho
kimetoa wito kwa wafugaji wote Tanzania kujihadhali na watu wanaopita
kwao na kujitambulisha kuwa wao ni viongozi wa chama cha wafugaji
Tanzania.
No comments:
Post a Comment