Mwakilishi
Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) Bw. Martin Kobler akiwafariji walinzi wa
amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) wanaohudumu katika
Misheni ya MONUSCO ( DRC) kufuatia shambulio lililotokea siku ya Jumanne
huko Ben,i Magharibi ya Jimbo la Kivu. Katika shambulio hilo na ambalo
limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu, Ban Ki Moon, walinzi wawili
wamepoteza maisha na wengine 13 wamejeruhiwa.
Na Mwandishi Maalum
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani vikali kuuawa kwa
walinzi wawili wa amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika Misheni ya
Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO).
Walinzi
hao wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na kundi la waasi
linalosadikiwa kuwa ni la Allied Democratic Forces ( ADF), shambulio
hilo limetokea siku ya jumanne katika eneo la Beni, Magharibi ya Jimbo
la Kivu ambapo walinda Amani wengine 13 wamejeruhiwa.
Shambulio
hilo limetokea wakati kikosi hicho cha walinzi wa Amani kutoka JWTZ
wakielekea kutoa ulinzi kwa wananchi na ndipo waliposhambuliwa
No comments:
Post a Comment