Na Editha Karlo
Waomba
hifadhi kutoka nchini Burundi wakiwasili nchini kwa boti hivi maeneo ya
Kibilizi, Mkoani Kigoma. Bado idadi yao haijafahamika kwani bado zoezi
la kuwaandikisha linaelea katika eneo hilo.Ujio wa waomba hifadhi hawa
unakuja kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Burundi ambayo
yameshika kasi na kusababisha wananchi kuanza kukimbilia nchini
Tanzania.
Burundi
ilikumbwa na machafuko katika miaka ya nyuma na baadaye kuwa na amani
lakini sasa inaingia katika mgogoro tena baada ya Rais wa sasa Pierre
Nkurunzima kutaka kuwania urais kwa muhula mwingine.
No comments:
Post a Comment