Watu watano
wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za
mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua
hizo zinazonyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya
watanzania hawa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama
ifuatavyo:
1. Mnamo
tarehe 06/05/2015 majira ya saa moja kamili usiku huko maeneo
ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu mmoja jina SHABAN S/O
IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng'ombe
alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku
iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa
katika hospitali ya Mwananyamala.
2. Kifo
kingine kilitokea tarehe 07/05/2015majira ya saa sita kamili mchana huko
maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay,
Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O
DOUGLASS @ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi wa Mwananyamala Mbuyuni,
alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji yaliyoingia
nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na
tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa
huo ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa
msaada wa haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya
Mwananyamala kwa uchunguzi
No comments:
Post a Comment