Thursday, June 4, 2015

Vilio vyatawala bungeni kifo cha Mwaiposa



Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa ukiwasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa jana. (Picha na Mohamed Mambo).
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa ukiwasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa jana. (Picha na Mohamed Mambo)
WABUNGE jana walikuwa na wakati mgumu kuzuia machozi kutiririka katika nyuso zao wakati jeneza lililobeba mwili wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, Eugen Mwaiposa lilipokuwa likiingia katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya mazishi.

Wengi wao wakiwa wamevalia vazi jeusi ikiwa ni alama ya maombolezo na wengine, hasa wanawake kuvalia khanga, waliangua vilio wakati mwili huo ukiingia viwanjani ukiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM) aliyekuwa amebeba msalaba.
Haukuwa uso tu wa Bulaya ulioonesha kutatizwa, bali na mwili wake wote haukuwa sawa sawa, ukionesha kubeba majonzi makubwa kwa msiba huo.

No comments:

Post a Comment