Thursday, June 4, 2015

Tendo la hisani la Wapendelevu’89 kwa Ocean Road Cancer Institute



Wapendelevu’89 ( WaP89) ni kikundi cha Wanawake waliomaliza Kidato cha sita Mwaka 1989 katika Shule ya Wasichana Weruweru. Kikundi hiki kinaundwa na wanachama 44 ambao wanajishughulisha na ujenzi wa Taifa katika Nyanja mbalimbali wakiwamo madaktari, wahasibu, wahadhiri, wachumi, walimu/wahadhiri na wafamasia.

Awamu ya pili ya ugawaji wa nguo kwa wagonjwa katika Wodi ya Wanawake. Mh. Al Shaymaar Kwegyir akisubiri mzigo wake wa kugawa huku akipata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa WaP89 Stella ¬Emma Katende ( katikati)
Akina mama wanachama wa WaP89 wakiwa na mgeni rasmi Mbunge wa Viti maalum Mh. Alshaymaar Kwegyir ( mwenye miwani) na Mwakilishi wa Wizara ya Afya ( Idara ya Magonjwa Yasiyoambukiza), Dr Shadrack Busweru ( mwenye shati Jeupe) wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Kikundi cha WaP89 kwa hospitali ya Ocean Road, Dar Es Salaam hivi karibuni

No comments:

Post a Comment