Watu
ambao tayari wamejitokeza kutangaza kwamba Wanagombea nafasi ya kuwa
wawakilishi wa CCM kwenye nafasi ya Urais idadi yao ni zaidi ya 35 mpaka
sasa hivi... Waziri Steven Wasira amewasha kipaza sauti ndani ya Kikao
cha Bunge Dodoma na kuongea hizi sentensi zake chache tu kwa wanaokosoa
idadi hiyo ya Wagombea.
“Chama
cha Mapinduzi ni Chama kikubwa wengine wako huko wananung’unika ooh
kina Wagombea wengi mlitaka wawe wachache ili wawe wangapi? Ni wengi kwa
sababu Chama chenyewe ni kikubwa, sio Chama kidogo ambacho Viongozi
wake wakiingia kwenye Helicopter chini kunabaki hakuna Kiongozi” Steven
Wasira.
“Tunapashapasha
moto alafu mwisho wa yote tunapata Mgombea mmoja na tutasonga mbele,
mwendelee kujiandaa kuwa Wapinzani” Waziri Steven Wasira.
No comments:
Post a Comment