Tuesday, June 23, 2015

Collabo za Baraka Da Prince na mastaa wakubwa Afrika




.
Baraka Da prince ambaye ni mshindi wa tuzo ya msanii bora chipukizi mwaka 2015 kwenye tuzo za KILI, time hii anakuja na collabo atakazo washirikisha wasanii wa Afrika Mashariki, Nigeria na Ghana.

Akizungumza na millardayo.com amesema ‘Kuna nyimbo nyingi zinakuja ambazo nimewashiriki kama Jose Chameleone, Jaguar na msanii kutoka Nigeria lakini siko tayari kumtaja jina lake ila mashabiki wake tayari kwa ujio wangu mpya,kwasasa niko Mwanza kwa wazazi ila mipango yangu ya kuachia single mpya mpaka nikirudi Dar es Salaam baada ya mwezi wa Ramadhani kuisha ndio kila kitu kitakuwa tayari hewani’alisema Baraka

No comments:

Post a Comment